Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaja sababu zilizomfanya kutomuunga mkono Naibu Rais William Rutto katika kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.

Kwa mujibu wa Gazeti la Sunday Standard limesema kuwa Rais Kenyatta amefichua kuwa Ruto alikuwa na njama ya kumwondoa madarakani katika muhula wake wa pili.

Katika mkutano wa wazee wa jamii ya Kikuyu katika Ikulu ya Nairobi, Uhuru anaripotiwa kuwaambia wazee hao kuwa Ruto alimwambia amruhusu kuendesha chama cha Jubilee ili naye aendeshe serikali.

Naibu Rais anadaiwa kutumia fursa hiyo kuvuruga kura za mchujo za Jubilee mwaka 2017 na kuhakikisha kuwa wafuasi wake wengi wanaingia bungeni ili kufanikisha kumwondoa Rais Kenyatta madarakani.

Uhuru na Ruto hawajakuwa na ukaribu tangu kukamilika kwa uchaguzi wa mwaka 2017 na salamu za heri kati ya Rais Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga zilimsukuma Ruto pembeni hata zaidi.

Kwa mujibu wa Uhuru, amesema kuwa naibu William Ruto alikuwa na njama ya kuhakikisha kuwa anakosa uwezo wa kuendesha serikali na kulidhibiti taifa.

Rais Kenyatta anasisitiza ni kwa nini eneo la Mlima Kenya linastahili kupinga urais wa Ruto akionya kuwa huenda eneo hilo likajutia endapo litapuuza maelekezo wake.

Uhuru tayari ametangaza waziwazi kuwa anamuunga mkono mgombea wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga na wala sio naibu wake William Ruto akimtaja kuwa mwenye njaa ya mamlaka.

Ukraine yaomba silaha za NATO kuikabili Urusi
Waziri wa Elimu ashiriki mkutano wa kimataifa DOHA FORUM