Azimio la Umoja One la Mgombea urais wa Chama cha Muungano wa Kenya, Raila Odinga na mgombea mwenza wake, Bi Martha Karua wamewaonya wapiga kura wa Mlima Kenya kutomchagua Naibu Rais William Ruto, wakisema ana tatizo kudhibiti hasira yake.
Odinga na Bi Karua, ambao walikuwa na kampeni katika uwanja wa Rais Kenyatta Kaunti ya Kiambu, walisema DP Ruto ana nguvu na ushawishi katika eneo hilo lenye kura nyingi laminitis sio mtu sahihi kwao.
Kiongozi huyo wa Azimio, aliahidi eneo hilo kuwa atakamilisha miradi ambayo Rais Kenyatta alianzisha iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti lakini Odinga, ambaye alipitia Ruiru, Githunguri, Kabete na Gatundu Kusini, alisema washindani wake ni wafisadi.
“Ikiwa huwezi kumheshimu bosi wako ilhali mnaishi ofisi moja, vipi kuhusu Wakenya? Nchi haiwezi kuongozwa na mtu mwenye masuala ya hasira kwa sababu hujui anachoweza kuwafanyia wananchi wake. Ukihisi serikali uliyomo ni mbaya, basi ujiuzulu,” Bi Karua alisema akiwa Githunguri.
Hata hivyo, hatua hii inajiri ikiwa ni siku chache baada ya kanda iliyofichuliwa kumnasa DP Ruto akiongea ingawa kwa mzaha, jinsi alivyokaribia kumpiga kofi Rais Kenyatta ili kumshawishi kurudia uchaguzi wa urais kufuatia kubatilishwa kwa matokeo ya mwaka 2017.
Odinga alisema, atakabidhi jukumu la kupambana na ufisadi kwa Bi. Karua katika serikali yake, huku akianisha rekodi yake inayojulikana linapokuja suala la kupambana na ufisadi na kwamba kusalimiana kwake na Rais Kenyatta kulileta maendeleo Kiambu.
Aidha, amesema atahakikisha kunafanyika uboreshaji wa hospitali ya Githunguri ya level 5, ambayo ilikuwa imekwama kutokana na ukosefu wa fedha huku akitumia ziara yake ya Kiambu kuandamana katika madai ya mpango wa wizi wa kura.
“Sasa kuna jambo moja peke yake Junet ameongea leo mambo ya wale wenye njama ya kuiba kura Jamaa mmoja ametuma watu huko Greece kule wanachapisha kura…ili watu wachapishe kura ya ziada…waingize Kenya …wamechagua polling station kama 10,000 ndio…wapate milioni mbili ya ziada… hiyo ndio maana Chebukati anakataa manual register,” amesema Odinga.
Hata hivyo Odinga amesema, “Mtu mmoja amemtuma mtu Ugiriki ambako kura zinachapishwa ili waweze kuingiza karatasi za ziada za kupigia kura”.
Amesema “Wamechagua takriban vituo 10,000 vya kupigia kura ili waweze kupata kura milioni mbili za ziada. Ndiyo maana Chebukati anakataa sajili hiyo ya mwongozo.’’
Bw Odinga aliyasema halo katika eneo la Githunguri, akirejelea maneno ya katibu mkuu wa chama cha Azimio, Junet Mohamed aliyoyatoa wakati wa kunadi sera za chama chake na kuomba kura kwa Wananchi wa Kenya.