Mgombea mwenza wa urais wa Muungano wa Umoja wa Kenya, Martha Karua amemtaka Rais mteule, William Ruto kuacha kuwashawishi wanachama wa Azimio wajiunge kwenye kambi yake ya Kenya Kwanza, akisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Akizungumza katika msiba, uliotokea katika kijiji cha Kiandieri Kaunti ya Kirinyaga, Karua amesema Ruto anakiuka moja kwa moja Sheria ya Vyama vya Kisiasa kwa kuwarubuini baadhi ya wanachama hao ili waondoke katika umoja wao.

Amesema, “Ni bahati mbaya kwa mtu yeyote anayewania kuongoza nchi hii, na kwa mtu ambaye ni naibu wa rais wa serikali inayoondoka madarakani, kuvunja sheria za nchi na hakipaswi kunyamaziwa.”

Bi Karua alieleza kuwa, Sheria ya Vyama vya Kisiasa inayoelekeza kuundwa kwa miungano ya vyajma ina masharti ya wazi ambayo yanaongoza harakati za watu kutoka maeneo mengine ya miungano ya kisiasa.

“Kwa hivyo kwa naibu rais kuanza kuwashawishi watu, kuwashawishi kuondoka kwenye muungano bila masharti ya kisheria, ni maonyesho ya kutokujali au kutojua sheria ya nchi,” aliongeza.

Mbunge huyo wa zamani wa Gichugu, alizidi kumshutumu Ruto kwa kujifanya kutojua sheria kama kisingizio cha vitendo ambavyo alitaja kuwa vinaegemea kutoadhibiwa wakati si jambo la kweli kwa mtu ambaye ni kiongozi wa nyadhifa ya juu.

Shambulio Hotelini lauwa zaidi ya watu 10
Kenya: Mwananchi awasilisha pingamizi uapisho wa Ruto