Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amewataka watu wanaoamini wanaibiwa pesa kwa njia ya vifurushi via mitandao ya simu wajitokeze hadharani ili kueleza umma upotevu huo wa gharama unatokeaje.

Nape amesema hayo alipokuwa akizungumza katika kituo cha redio cha Clouds FM wakati akifanya mahojiano juu ya uzinduzi wa mnara wa mtandao katika mlima Kilimanjaro.

Nape amesema, “Nilitoa ofa kwamba kama kuna mtu anaamini ameibiwa aje atusaidie kupata ushahidi wa huo wizi, wapo wengi wamekuja, wakishafanyiwa tathmini hawataki kwenda public, na wengine ni viongozi. Ni vizuri kuwa makini na matumizi ya smart devices,”

Hata hivyo ameongeza kuwa bei ya vifurushi vya simu bado inaendana hali ya watanzania kwa sababu Nchi za wengine hali ya matumizi imeachwa huru kutokana na uchumi wa wao.

“Wenzetu walipofikia wameachia soko liamue lakini sisi tumesema tukiachia soko liamue watu watashindwa kumudu gharama za data, kwa hiyo tumezibana. Matumaini yetu ni kwamba kwa sababu kuna uwekezaji mkubwa umefanyika gharama zitakazobaki ni hizi za uendeshaji,” ameongeza Nape.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

“Inawezekena bei tunayouzia data ni ya chini ukienda nchi kama Afrika Kusini, Uingereza, Canada kwa sababu uchumi wao ni mkubwa, sisi bado watu wetu ni masikini na ndio maana kama Serikali tunachofanya ni kudhibiti tusipande sana,”

Waziri Nape pia ametoa wito kwa Wananchi na watumiaji wa mitandao kuhoji kwa utaratibu na kuweta hasira pembeni ili kupata ufafanuzi mzuri na wa staha.

“Nitoe wito kwa TCRA na makampuni ya simu, mimi kazi yangu ilikuwa ni kuanzisha huu mjadala kazi yao ni kujibu maswali ya Watanzania, waendelee kuwaelimisha juu ya jambo hili, tuendelee kujadiliana naamini mwishoni tunaweza kutoka na kitu kizuri,” Nape.

“Kanuni na sheria za Mamlaka ya Mawasiliano nchini haimruhusu mtoa huduma kupandisha huduma bila kupeleka kwa mamlaka, ukisharuhusiwa kabla ya kutekeleza lazima utaarifu umma, bahati mbaya iliyopo ni kwamba wanazituma watu hawazioni, ikipanda ndio wanasema hawakuambiwa.” Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Kenya: Mwananchi awasilisha pingamizi uapisho wa Ruto
Seneta wa Marekani aeleza 'alichoteta' na Rais Kenyatta