Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa pongezi kwa wahanga wa ugaidi, kuadhimisha siku ya kimataifa iliyoanzishwa ili kuhakikisha kuwa waathirika na walionusurika wanasikilizwa kila wakati na kutosahaulika.
Guterres ameyasema hayo na kudai kuwa, kila mwaka, vitendo vya kigaidi vimekuwa vikidhuru na kuua maelfu ya watu wasio na hatia, licha ya uangalizi wa kimataifa ambapo mara nyingi watu walioathirika hutatizika kupata huduma muhimu za kimwili, kisaikolojia, kijamii na kifedha.
Mhanga wa Mlipuko wa Bomu kwenye Hoteli ya Canal nchini Iraq mwaka 2003, Laura Dolci katika tukio lililowauwa Wafanyakazi 22 wa Umoja wa Mataifa na zaidi ya 100 kujeruhiwa, amesema, “Wapo maelfu ya waatharika wa ugaidi na familia zao, waliotawanyika katika maeneo yote ya dunia, wakijitahidi kuishi katika upweke na majeraha.”
Kukumbuka, na kutoa heshima kwa waathirika wa ugaidi kuna chukua jukumu kuu katika kuonyesha kwamba hali yao kama wathirika inaheshimiwa na kutambuliwa, huku mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuhusu matibabu ya waathiriwa wa ugaidi, ukiwakilisha kipengele muhimu cha mkakati wa Kimataifa wa Kupambana na Ugaidi wa shirika hilo.
Siku hiyo kwa mwaka huu inaenda sambamba na maadhimisho ya Dunia kutoka kwenye dharura ya afya ya umma iliyosababishwa na janga la Uviko-19, ugonjwa unaoongeza mapambano ambayo tayari yanakabiliwa na waathirika wa ugaidi.
Kaulimbiu ya Siku hiyo iliyochaguliwa kufuatia mashauriano na waathiriwa, ni “kumbukumbu huunganisha watu pamoja na kuashiria ubinadamu wetu wa kawaida kwa upande wa ugaidi, ikiunganishwa na hasara na maumivu katika jamii na kuruhusu kubadilishana mawazo ikiwemo kutoa suluhu zinazolengwa.