Nahodha wa Maafande wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile ameitaka Simba SC kuwa tayari kwa mchezo wa kesho Jumatano (Septemba 14), utakaopigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Asukile ametoa tahadhari hilyo alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne (Septemba 13) majira ya Mchana jijini Mbeya, ambapo amesema kikosi chao kimejiandaa kikamilifu kuikabili Simba SC, huku kikiweka dhamira ya kushinda kwenye uwanja wa nyumbani.

Mchezaji huyo mwenye sifa ya kucheza kama KIRAKA anapokua uwanjani amesema wanafahamu Simba SC imetoa kucheza mchezo wa Kimataifa na kushinda ugenini, lakini hilo haliwasumbui kwa sababu kitakachowapeleka Uwanjani kesho ni Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tunafahamu Simba SC imetoka Kimataifa na imeshinda huko ilipokuwa, hili halitusumbui kwa sababu kesho tunakwenda kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara, dhamira yetu kubwa ni kuutumia vizuri Uwanja wa nyumbani ili tupate alama tatu.”

“Tunajiamini hilo linawezekana kwa sababu tuna kikosi imara na kilicho tayari kucheza mchezo wa kesho, hivyo tuwanasisitiza mashabiki wetu waje kutupa ushirikiano ili tukamilishe kazi ya kuzibakisha alama tatu nyumbani.” amesema Asukile

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana msimu uliopita katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Simba SC ilikubali kupoteza kwa 1-0, bao likifungwa na Benjamin Asukile.

Juma Mgunda achimba mkwara mzito Simba SC
Tshabalala, Mwamnyeto watemwa Taifa Stars