Viongozi wa Umoja wa Ulaya EU, wamekubaliana kuhusu hatua zitakazochukuliwa wiki zijazo za kuwalinda raia kutokana na ongezeko la bei ya nishati.
Makubaliano hayo, yaliafikiwa baada ya saa 11 za mazungumzo yaliyotawaliwa na tofauti kuhusu mapendekezo yaliyowasilishwa, ya kupunguza bei ya gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari, rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema makubaliano ya mkutano huo wa kilele yameweka ramani Madhubuti ya kuendelea kufanyia kazi suala la bei ya nishati.
Kupanda kwa bei ya nishati barani Ulaya kumesababishwa zaidi na vita vya Ukraine.