Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari ameshiriki majadiliano yanayoendelea kuhusu changamoto za utoaji wa huduma za Mawasiliano, katika awamu ya nane (8) ya mijadala inayofanyika kwenye Kongamano la sita (6) la TEHAMA linaloendelea Visiwani Zanzibar.
Mjadala huo utakaoendelea hadi Oktoba 28,2022 pia unazungumzia namna Teknolojia inavyoendelea kuboresha utoaji wa huduma bora za Mawasiliano pamoja na upatikanaji wa huduma mpya za kidijitali.
Dkt. Jabir amesema “tuko hapa kuunga mkono na kufanya mambo yatokee na changamoto zipo na zitatatuliwa na ndio maana tuko hapa.”
Washiriki wengine katika mjadala huo ni pamoja na TISPA, Liquid Intelligent Technologies baadhi ya makampuni ya simu na ISOC Tanzania.