Rais wa Heshima na Mwekezaji Mwenza wa Klabu ya Simba SC Mohemd Dewji Mo ameipongeza timu ya Simba Queens kwa kufanikiwa kutinga Nusu Fainai ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba Queens ilikamilisha safari ya kutinga hatua hiyo juzi Jumamosi (Novemba 05), kwa kuifunga Green Buffalo ya Zambia mabao 2-0, katika mchezo wa mwisho wa Kundi A.

Mo ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwa kuandika: Hongereni sana @simbaqueensctz, kwa kufanikiwa kufika Nusu fainali ya Ligi ya Wanawake ya Mabingwa Afrika, kwa mara ya kwanza katika Historia! Umetufanya tujivunie sana. Nusu fainali tunakuja! #NguvuMoja #CAFWCL

Hata hivyo mapema leo Jumatatu (Novemba 07), Simba SC imeweka ujumbe huo katika kurasa zake za Mitandao ya Kijamii ikiwa ni kama msisitizo wa kilichoandikwa na kiongozi huyo wa heshima.

Simba Queens itacheza mchezo wa Nusu Fainali keshokutwa Jumatano (Novemba 09) na Mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoongoza msimamo wa Kundi B.

Wenyeji AS FAR nayo itacheza Nusu Fainali dhidi ya dhidi ya Bayelsa Queens ya Nigeria iliyomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B.

Michuano hiyo itafikia tamati Jumapili (Novemba 13) kwa washindi wa michezo ya Nusu Fainali kukutana kwenye mchezo wa Fainali, utakaopigwa katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo mjini Rabat.

Timu zitakazopoteza katika Hatua ya Nusu Fainali zitacheza mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu na wa nne Jumamosi (Novemba 12), katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo mjini Rabat.

Bodi ya ushauri kuipeleka Tanzania AFCON 2027, Kombe la Dunia 2030
Vikao changamoto za Muungano kuendelea