Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema vikao vya kupokea na kujadili changamoto za Muungano vitaendelea kuwepo kutokana na umuhimu wake katika mustakabali wa Taifa.

Naibu Waziri Khamis ameyasema hayo hii leo Novemba 07, 2022 jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mwera, Zahor Mohammed Haji aliyetaka kufahamu uwepo wa vikao vya kupokea na kujadili changamoto za Muungano, na vilikaa lini mara ya mwisho.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis.

Akiendelea kujibu swali hilo, Khamis alisema vikao hivyo hufanyika kwa mujibu wa mwongozo wa utaratibu wa vikao vya Kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), ya kushughulikia masuala ya Muungano ulioridhiwa na pande zote mbili.

Amesema, kwa mwaka 2021/22 vikao hivyo vilifanyika kwa mujibu wa mwongozo huo na kikao cha kamati ya pamoja ya SJMT na SMZ ya kushughulikia Masuala ya Muungano kilifanyika Agosti 24, 2021, na kwamba hoja 11 kati ya 18 zilipatiwa ufumbuzi na kuondolewa kwenye orodha ya hoja za Muungano.

Simba SC yakazia salamu za Mo Dewji
Moses Phiri: Mgunda amenipa siri ya mabao