Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amesema kuwa msukumo anautoa Rais Samia Suluhu Hassan, uwepo wa vyombo ya kiuwakajibikaji na Serikali kuridhia Mpango wa Afrika wa Kujitathimini (APRM), kwa pamoja vinachochea uwazi hapa nchini.

Ndejembi ameyasema hayo hii leo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Grace Tendega ambaye alihoji sababu za serikali kujiondoa kwenye Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) na katika maswali ya nyongeza, mwanasiasa huyo alitaka kujua lini serikali itarudi katika mpango huo.

Amesema, uwepo wa vyombo kama Tume ya Haki za Binadamu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na msukomo binafsi anaoutoa Rais wa Nchi kwa pamoja vinachangia uwazi na uwajibikaji.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi.

Amevitaja vyombo vingine vinavyochochea uwazi na uwajibikaji kuwa ni Utawala Bora, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Utumishi wa Umma.

Katika ngazi ya kimataifa, Naibu Waziri amesema kuwa Serikali imeendelea kuwa moja ya nchi zilizoridhia mfumo wa kukaguana wa nchi za kiafrika APRM (African Peer Review Mechanism) ambao ulianzishwa mwaka 2003 na Kamati ya Wakuu wa Nchi za Kiafrika.

Maaskofu watuhumiwa unyanyasaji wa kingono
Serikali yatoa taarifa hali za majeruhi ajali ya Ndege