Viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa wamefichua kuwa maaskofu 11 wa zamani nchini humo, akiwemo Kadinali walifanya unyanyasaji wa kingono bila tukio hilo kuripotiwa.

Msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa, Eric de Moulins-Beaufort, amesema kutokana na tukio hilo, baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa kanisa, walihukumiwa katika Mahakama za uhalifu, au za Kanisa.

Aidha, Kadinali Jean-Pierre Ricard ambaye alikuwa askofu wa muda mrefu wa jimbo la Bordeaux mmoja wa Viongozi wa Kanisa binafsi amekiri kumnyanyasa kingono msichana mwenye umri wa miaka 14, miaka 35 iliyopita.

Hata hivyo, Msemaji wa Baraza la Maaskofu la Ufaransa na Askofu wa jimbo la Reims, amesema maaskofu wote waliohusika na uhalifu huo wa unyanyasaji wa kingono watawajibishwa.

Polisi yatoa angalizo matumizi vyombo vya moto
Ndejembi amtaja Rais samia uwajibikaji na uwazi