Serikali nchini, itaendelea kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu ili wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi wanufaike na maeneo hayo kwa kuendesha shughuli za utalii badala ya kulima mazao yanayopendwa na wanya.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa kikao cha nne cha Kamati Tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara.

Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha  akizungumza wakati wa kikao cha nne cha Kamati  ya Usimamizi  wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara.

Amesema “Wizara ya Maliasili na Utalii imejidhatiti katika kuhakikisha kuwa migongano kati ya binadamu na wanyamapori inadhibitiwa kabla ya kuleta madhara, ili wananchi wafurahie uwepo wa wanyamapori.”

Sedoyeka ameongeza kuwa, wananchi wakinufaika na shughuli za uhifadhi watawafichua majangili kabla hawajaleta madhara, hivyo Wizara itahakikisha wanyamapori wakali na waharibifu hawaathiri maisha ya wananchi.

Viongozi na Wajumbe katika picha ya pamoja, wakati wa kikao cha nne cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo.

Awali, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha nne cha Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara haramu ya nyara, Christine Musisi alisema suala la kupunguza migongano kati ya Binadamu na Wanyamapori linahitaji ushirikiano wa Serikali na wananchi.

Amesema, mradi huo utaendelea kuzinufaisha jamii kufanya shunguli zingine za kiuchumi na kuachana na vitendo vya ujangili kwa kutoa mafunzo mbalimbali ya kuwakwamua kutoka kwenye umaskini.

Nabi kufumua mipango ya Club Africain
Fei Toto awaomba msaada mashabiki