Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, linatarajiwa kupiga kura ya azimio linalotaka Urusi kuilipa fidia Ukraine, kutokana na majeraha sambamba na uharibifu wowote uliosababishwa na matendo yanayotambuliwa kuwa ni makosa ya kimataifa.

Robo tatu ya mataifa 193 wanachama wa Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa yalipiga kura mwezi Machi mwaka huu (2022), kulaani uvamizi wa Urusi na kisha baadaye mwezi Oktoba kulaani jaribio la Moscow kunyakua baadhi ya maeneo ya Ukraine.

Mmoja wa Askari akiwa ameziba masikio wakati wa mashambulizi katika vita inayoendelea nchini Ukraine. Picha ya Dimitar Dilkof/ AFP.

Haya yanajiri wakati Rais wa Ukraine, Volodymyrr Zelenskiy akisema Ukraine haitaachia hata sentimita moja katika mapambano ya kudhibiti mkoa wa mashariki wa Donetsk, huku mawakala wa Urusi wakisema vikosi vya Ukraine vinaelekea kusini kwa vifaru.

Vikosi vya Ukraine, vimekuwa kwenye mashambulizi katika miezi ya karibuni, huku Urusi ikijipanga kutetea maeneo ya Ukraine inayoendelea kuyakalia, baada ya kuwaita mamia ya maelfu ya askari wa akiba katika kipindi mwezi mmoja uliyopita.

Firmino afunguka kuachwa Kombe la Dunia
Nabi kufumua mipango ya Club Africain