Baada ya kutemwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2022 baadae mwezi huu nchini Qatar, Mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool Roberto Firmino amefunguka kwa mara ya kwanza.

Kocha Mkuu Adenor Leonardo Bacchi ‘Tite’ juzi Jumatatu (Novemba 07) alitangaza kikosi cha wachezaji 26, ambapo anaamini kitaweza kutetea Taifa la Brazil kwenye Fainali za mwaka huu.

Roberto Firmino amesema amesikia na kupokea kwa mikono miwili maamuzi ya mwisho ya Kocha ‘Tite’, hivyo atakuwa mtazamaji na kuiombea mema timu yake ya Taifa itakapokua Qatar.

Firmino amesema alitamani kuwa sehemu ya kikosi hicho kutokana na hitaji la kuitetea nchi yake, lakini anaamini ‘mambo hayakwenda’ kama alivyotarajia.

Amesema kuwa ‘hakuwaza’ kama angetemwa lakini hakuna sababu ya kulalamika zaidi anamshukuru Mungu na kuwapongeza walioteuliwa katika hiko kitakachoeleka Kombe la Dunia nchini Qatar.

“Mambo hayakwenda kama nilivyowazia au nilivyoota maisha yangu yote lakini natazama nyuma na nabaki kumshukuru Mungu kwa sababu tayari ameniruhusu kuishi ndoto hii mnamo 2018”

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wote walioitwa.” Ameandika Roberto Firmino katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Kikosi cha wachezaji 26 kilichotajwa na Kocha ‘Tite’ juzi Jumatatu Walinda Lango ni Edouard Mendy, Alfred Gomis na Seny Diang

Mabeki: Bouna Sarr, Saliou Ciss, Kalidou Koulibaly, Pape Abou Cisse, Abdou Diallo, Ibrahima Mbaye, Abdoulaye Seck, Fode Ballo Toure na Cheikhou Kouyate

Viungo: Pape Matar Sarr, Pape Gueye, Nampalys Mendy, Idrissa Gana Gueye, Moustapha Name, M. Loum Ndiaye, Joseph Lopy.

Washambuliaji: Sadio Mane, Ismaila Sarr, Bamba Dieng, Keita Balde, Habib Diallo, Boulaye Dia, Famara Diedhiou na Mame Babe Thiam

Kombe la Dunia 2022: Sadio Mane azua hofu Senegal
Wapiga kura Urusi ilipe fidia uharibifu Ukraine