Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans Kostadin Papic ameendelea kushangazwa na Mpango wa Klabu za Simba SC na Young Africans kuendelea kuwatumia wachezaji wengi wa kigeni.
Klabu hizo nguli za Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa muda sasa zimekua na Rundo la Wachezaji wa Kigeni kwa kuzingatia Kanuni za Usajili Tanzania Bara ambapo klabu zinaruhusiwa kusajili Wachezjai wa Kigeni 12.
Papic amesema Klabu hizo zinapaswa kujitafakari kwa kina ili kuamini zinaweza kujiendesha kwa kuwa na wachezaji wengi wazawa ambao wataweza kuzifikisha mbali katika MIchuano ya ndani na nje ya Tanzania.
“Mimi nashangaa kwa nini Simba SC na Young Africans wanawachezaji wengi wa kigeni inaonyesha ni kama hawaamini wachezaji wa kitanzania, mimi nataka kuwahakikishia kuwa Tanzania kuna vijana wenye vipaji wapewe nafasi za kucheza.
“Nakumbuka kwenye Young Africans yangu, wote mnakumbuka walikuwa wachezaji wa Kitanzania tu, Hakuna aliyewakumbuka wachezaji wa kigeni, mnakumbuka Chuji, Shedrack, Tegete mnakumbuka wote walikuwa Watanzania,” amesema Papic