Viongozi wa upinzani nchini DRC, akiwemo mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2018, Denis Mukwege wameushutumu utawala wa Rais FĂ©lix Tshisekedi kwa kutekeleza sera ya kutumia vikosi vya nje kwa usalama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku nchi ikitishiwa na hali mbaya ya usalama.

Viongozi hao akiwemo pia Augustin Matata Ponyo na Martin Fayulu, wamesema kupitia taarifa yao waliyoisambaza kuwa, DRC ipo katika hatari ya kutumbukia katika mzozo mkubwa, kutumiwa na mataifa ya kigeni kutokana na matokeo ya mapungufu ya uongozi na utawala usiowajibika na kandamizi.

Waziri Mkuu wa zamani wa DRC (2012-2016), ambaye sasa ni Seneta, Augustin Matata Ponyo. Picha ya Frederico Scoppa, AFP.

Fayulu, ambaye ni mgombea urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa mwaka 2018 na kulalamikia matokeo na ambaye bado anadai zaidi ya asilimia 60 ya kura, wametoa madai hayo pamoja na Ponyo ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani (2012-2016), akiwa ni Seneta kwasasa aliyewahi kukabiliwa na kesi ya madai ya ubadhirifu.

Taarifa yao imebainisha kuwa, “Badala ya kuipatia nchi jeshi lenye ufanisi,” wanabainisha, serikali imependelea sera ya kutoa usalama wa taifa kwa vikosi vya kigeni na, mbaya zaidi, kwa mataifa ambayo ni chanzo cha kuhatarisha usalama wa nchi ikiwemo Rwanda na Uganda.”

Prof. Mbarawa ataja maelekezo ya Rais Samia
Mwinyi alia na changamoto mahitaji ya chakula