Ujenzi wa barabara ya Ibanda hadi Kajunjumele iliyopo Kyela Mkoani Mbeya, yenye urefu wa kilomita 22 utakaojengwa kwa gharama ya Shilingi 38.35 bilioni huku ujenzi wake ukitarajia kukamilika ndani ya miaka miwili, umetajwa kuwa utafungua fursa za kiuchumi na usafirishaji nchini.

Hayo, yamebainishwa na hii leo Desemba 27, 2022 na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Rogatus Mativila katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi huo na ile inayoanzia Kajunjumele kuelekea Itungi Port ya km 4 na Kajunjumele hadi Kiwira Port yenye urefu wa km 6.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Rogatus Mativila.

Amesema, “Usanifu wa Barabara hii ulianza kwa upembuzi yakinifu kuandaa nyaraka za zabuni tangu mwaka 2017 na ulikamilika mwaka 2019 na barabara hii ni muhimu kwani inaunganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma kupitia Ziwa Nyasa na bandari za Itungi, Kiwila na Mbamba Bay.”

Amesema katika kuchochea shughuli za kiuchumi, usafirishaji wa mazao mbalimbali utafanyika na kuwa kiungo muhimu kwa barabara kuu kutoka Mbeya kwa kuunganisha nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia na Zimbabwe huku akisema “Barabara hii pia inaunganisha hadi Mtwara ambako kuna bandari, ikijengwa hii pia itaunganisha Songea, Mtwara bandarini.”

Liverpool yafunguliwa mlango kwa Cody Gakpo
Jose Mourinho aikacha Navegadores (The Navigators)