Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wibroad Mutafungwa, amethibiti kutokea kwa tukio la kujinyonga hadi kufa kwa mkazi wa Kiseke Manispaa ya Ilemela, Swadika Abasi (50) aliyetumia mtandio kujining’niza kwenye kenchi la paa la nyumba yake.

Mutafungwa ameyasema hayo, Desemba 25, 2022 na kuongeza kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 17, 2022 Mtaa wa Zenze uliopo Kata ya Kiseke Manispaa ya Ilemela muda mfupi baada ya Swadika kutoka kufunga ndoa na mkewe Elieth Rwegoshera (40), katika msikiti wa Swadikil Amiin Kiseke.

Amesema, baadaye walitarajia kwenda kufanya sherehe fupi katika ukumbi wa Mtena B ulioko Buzuruga, ambapo hadi kufikia majira ya saa nne usiku mwanamume huyo aliyekuwa akisuburiwa hakutokea ukumbini.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wibroad Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amefafanua kuwa, “Ilibidi sasa atafutwe na walipokwenda nyumbani kwake walikuta amejinyonga kwa mtandio huku mwili wake ukiwa umening’inia kwenye kenchi na ndipo ilipotolewa taarifa kuhusu tukio hilo.”

Aidha, ameongeza kuwa, katika uchunguzi wa awali walipatikana kipande cha karatasi chenye ujumbe wa kujiua unaohifadhiwa kwa sasa kwa ajili ya upelelezi na uchunguzi na kuwataka ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa watulivu wakati polisi wakiendelea na upelelezi wa tukio hilo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 27, 2022
Mwandishi wa Habari aliyegoma kula alazwa Hospitali