Mwandishi wa habari na mkosoaji wa serikali ya Senegal, Pape Ale Niang, ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula kupinga mashtaka dhidi yake amehamishiwa hospitalini baada ya afya yake kuzorota. 

Kwa mujibu wa taarifa ya mmoja wa mawakili wake, Dakar Matin amesema Niang, ambaye ni mkuu wa tovuti ya Habari za mtandaoni aligoma toka Desemba 2, 2022 baada ya kuwa kizuizini kwa wiki kadhaa. 

Mwandishi wa Habari, Pape Ale Niang. Picha ya Article 19.

Amesema, hali yake ilipokuwa mbaya alilazwa hospitali na baadaye aliachiliwa kwa muda kabla ya kukamatwa tena Desemba 20, 2022 na awali alikamatwa Novemba 6, 2022 na kushtakiwa kwa kufichua habari zinazoweza kuhatarisha usalama wa taifa. 

Kesi dhidi yake iliibuka baada ya kuandika kuhusu mashtaka ya ubakaji yanayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Ousmane Sonko ambaye alishutumiwa Vivaldi na umma juu ya tukio hilo.

Ajinyonga muda mfupi baada ya kufunga ndoa
Boti yazama, 180 wahofiwa kufa maji