Jumla ya watu 180 wa kabila la warohingya waliokwama baharini kwa wiki kadhaa baada ya kuondoka Bangladesh, wanahofiwa kufa kufuatia boti waliyokuwa wakisafiria kuhofiwa kuzama. 

Shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa UNHCR, limeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba watu hao walipoteza mawasiliano na jamaa zao, huku ikizitaka nchi za eneo hilo kusaidia kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu.

Moja Kati ya ajali za boat zilizopoteza maisha ya watu wengi nchini Nigeria. Picha ya CT.

Zaidi ya wakimbizi milioni 1 wa Rohingya kutoka Myanmar wanaishi katika kambi zilizojaa, huku wengi wao wakiwa ni waislam kutoka Bangladesh na wengi wao walikimbia Myanmar baada ya jeshi kufanya ukandamizaji 2017. 

Kundi la waislamu wa warohngya, wamekuwa wakinyanyapaliwa nchini Myanmar yenye wakazi wengi wa dini ya Budha, na hivyo kulazimika kufanya safari za hatari kuelekea nchi za kusini mashariki mwa Asia ,kwa ajili ya kutafuta hifadhi na maisha bora. 

Mwandishi wa Habari aliyegoma kula alazwa Hospitali
Ukraine yawaonya raia wake mashambulizi ya Urusi