Halmashauri ya Jiji la Dodoma imezika jumla ya maiti 59 zilizopokelewa katika kipindi cha Januari hadi Desemba 19, ambazo zimekosa ndugu wa kuzima heshima za mwisho na kuwapa pumziko.

Hatua hiyo, imethibitishwa Desemba 26, 2022 na Ofisa Afya Usafishaji wa Jiji la Dodoma, John Lugendo ambaye amebainisha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 19, 2022 tayari wamezika miili 59 ya marehemu waliokosa ndugu zao.

Amesema, mwezi wa Desemba ulikuwa na maiti 12 na Januari zilikuwa nne pekee na kwamba katika miezi ya Februari, Aprili, Julai na Septemba hawakuzika miili yeyote ingawa kwa mwezi Machi, Juni, Agosti na Novemba walizika miili saba na mwezi Oktoba wakizika miili minane pekee.

Mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti, akikagua miili katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Joe Simon nchini Afrika Kusini. Picha ya Jonathan Lestrade.

Lugendo amesema, “Maiti nyingi zinaozikwa na jiji ni za vijana ambao hufariki kwa ajali au kuugua na baadhi ya miili tunaikuta ikiwa na majeraha makubwa yanayohisiwa ni ya risasi au mapanga hasa vijana wenye umri kati ya miaka 25 hadi 35.”

Hata hivyo ameongeza kuwa, miili mingine huhifadhiwa kutokana na kukosa ndugu hasa jamii ya wafugaji na wengine kuiogopa miili ya ndugu zao kutokana na matukio ya uhalifu ambayo yalifanywa na marehemu enzi za uhai wao.

Idadi waliokufa na theluji yafikia watu 50
Tshisekedi kugombea tena urais