Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi anatarajiwa kugombea tena urais baada ya muhula wa kwanza, ambapo tajari nchi hiyo imeanza usajili wa wapiga kura ili kujiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Desemba 2023.

Tume ya Uchaguzi (CENI) ilizindua mfumo mpya wa usajili wa awali wa simu za rununu ili kuharakisha mchakato na kuzuia misururu mirefu iliyojitokeza wakati wa uchaguzi uliopita.

Takriban watu milioni 50 katika majimbo 26 ya taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati wanatarajiwa kujiandikisha kupiga kura katika muda wa miezi mitatu ijayo ambapo uandikishaji huo umeanza Desemba 23, 2022.

Lakini vituo vingi vya usajili katika mji mkuu, Kinshasa, vilishindwa kufunguliwa kama ilivyopangwa kutokana na ukosefu wa wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Reuters Muangalizi wa uchaguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema ni vifaa 6,900 pekee kati ya zaidi ya 11,000 vinavyohitajika kwa awamu ya kwanza ya usajili viliwasili mwanzoni mwa wiki iliyopita.

“Ni kama gari, unaanza kwa gia ya kwanza, hauendi moja kwa moja kwenye gia ya tatu,” Mwenyekiti wa CENI Denis Kadima alisema baada ya kujiandikisha mjini Kinshasa.

Tshisekedi (59), pia alisajiliwa Jumamosi katika mji wa kaskazini magharibi wa Mbandaka, ambapo mlipuko wa Ebola ulitokea mapema mwaka huu.

Kiongozi wa upinzani Moise Katumbi ambaye ni gavana wa zamani mwenye nguvu wa jimbo la Katanga linalozalisha shaba, pia ametangaza kugombea nafasi ya urais.

Maiti zilizokosa ndugu, jamaa zazikwa rasmi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 27, 2022