Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la mvua kubwa zinazoweza kuleta madhara zinazotarajia kunyesha katika mikoa 11 ya Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa TMA kuhusu matarajio ya hali hiyo ya Hewa, imeeleza kuwa Mikoa hiyo ni Njombe, Morogoro, Mbeya, Songwe, Ruvuma, Rukwa, Singida, Iringa, Dodoma, Lindi na Mtwara.
Tarifa hiyo imedai kuwa, athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji sambamba na ucheleweshwaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na usafirishaji.