Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kusimamia na kuendeleza kampeni ya “Soma na Mti” kwa kuhakikisha kila shule na kila mwanafunzi anakua na  Mti wake bila kujali kiwango cha elimu.

Senyamule ametoa agizo hilo, wakati alipokua akiongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), kilichopo Ihumwa katika kampeni aliyoizindua ya upandaji miti kwa Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akishiriki zoezi la upandaji miti eneo la Ihumwa.

Amesema, “Leo tupo hapa kutekeleza mpango wa Serikali juu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni mwendelezo wa juhudi zilizoanzishwa na wenzetu. Nitoe rai kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha tunasimamia maelekezo ya Serikali ya kuzuia ukataji miti bila vibali, na kupanda miti.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa pia amesisitiza kufuatwa kwa Sheria ndogo ndogo zilizowekwa na Jiji la Dodoma kwa kila Kaya kupanda miti mitano kwenye eneo lake, na  kuongeza kuwa kila anayenunua eneo ahakikishe amepanda idadi ya miti mitano. 

Wapinzani wapiga kura kuivunja Serikali
Papa Benedict XVI 95 amefariki dunia