Papa Emeritus Benedict XVI amefariki dunia akiwa na miaka 95, Vatcan imetangaza.

Kwa mujibu wa tovuti ya Vatican News, Papa Benedict amefariki leo Disemba 31, 2022 saa 3:34 akiwa katika makazi yake huko Vatican alipokuwa anaishi tangu kujiuzulu kwenye nafasi hiyo mwaka 2013.

Taarifa za kuugua kwake zilitolewa mapema wiki hii na Ofisi ya Habari kutoka Vatican juu ya kuzorota kwa hali ya kiafya cha chanzo kikitajwa ni changamoto ya umri.

Alijiuzulu nafasi hiyo mwaka 2013, akiwa Papa wa kwanza kufanya hivyo tangu Gregory XII alipojiuzulu mwaka 1415.

Katika taarifa yake Vatican imesema “Kwa masikitiko ninawajulisha kuwa Papa Mstaafu, Benedict XVI amefariki dunia leo saa 9:34 katika Monasteri ya Mater Ecclesiae huko Vatican.”

Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda usiozidi miaka minane, kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2013, akawa Papa wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII alipojiuzulu mwaka 1415.

Siku ya Jumatano, Papa Francis alitoa wito kwa hadhira yake ya mwisho ya mwaka huko Vatican kusali sala maalum kwa ajili ya Papa Benedict ambaye alisema alikuwa mgonjwa sana.

Mrithi wake Papa Francis alisema alikuwa anamtembelea huko mara kwa mara licha ya kwamba papa huyo wa zamani alikuwa mgonjwa kwa muda, Baraza Kuu lilisema kulikuwa na hali mbaya katika hali yake kwa sababu ya uzee. 

Joseph Ratzinger alikuwa na umri wa miaka 78 mwaka 2005 na akawa mmoja wa mapapa wakongwe kuwahi kuchaguliwa akipoewa jina la Benedicto XVI.

Kwa sehemu kubwa ya upapa wake, Kanisa Katoliki lilikabiliwa na madai ya kisheria na ripoti rasmi katika miongo kadhaa ya unyanyasaji wa watoto na makasisi.

Mapema mwaka huu Papa huyo wa zamani alikiri kwamba makosa yalikuwa yamefanywa katika kushughulikia kesi za unyanyasaji alipokuwa askofu mkuu wa Munich kati ya 1977 na 1982.

Papa Benedict ambaye jina lake kamili ni Joseph Ratzinger ni mzaliwa wa Ujerumani ambapo alitumia miaka yake ya mwisho katika monasteri ya Mater Ecclesiae ndani ya kuta za Vatican. 

Soma na Mti: Senyamule awapa maagizo Wakurugenzi
Rais mstaafu Mahakamani kwa utakatishaji fedha