Katibu Mkuu wa Shirika la Waandishi Habari wasio na Mipaka (RSF), Christophe Deloire amesema takribani waandishi habari 1,700 wameuwa duniani kote katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. 

Deloire, ameyasema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari na kuongeza kuwa, waliouawa ni wale waliojitolea maisha yao kwa ajili ya kukusanya taarifa, kufanya utafiti wa kupata ukweli na shauku yao ya uandishi habari huku akizutaja Iraq na Syria kama moja ya nchi ambazo ni hatari kufanya kazi za uandishi. 

Moja kati ya changamoto ambazo wanakutana nazo waandishi wa Habari. Picha ya Slovenia Times.

Amesema, jumla ya waandishi habari 578 wameuawa kwenye nchi hizo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na kwamba I dadi hiyo inafuatiwa na waandishi habari 125 waliouawa Mexico, 107 Ufilipino, 93 Pakistan, 81 Afghanistan na 78 Somalia. 

Aidha, kwa upande wa bara la Ulaya Uturuki imeshika nafasi ya tatu kama nchi hatari zaidi kufanya kazi za uandishi wa Habari, ikifuatiwa na Ufaransa kutokana na mauaji ya wafanyakazi wa jarida la vibonzo la Charlie Hebdo jijini Paris, mwaka 2015.

Rais mstaafu Mahakamani kwa utakatishaji fedha
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 31, 2022