Sehemu ya mapato ya ndani ambayo Uganda inatumia kulipia deni lake la umma imepanda hadi asilimia 30  tangu Oktoba, 2022 kutoka asilimia 24 kwa kipindi kama hicho miaka miwili iliyopita hali inayoweka shinikizo lisilofaa kwa fedha za umma.

Katika ripoti ya utendaji wa uchumi, Benki Kuu ya Uganda inasema ulipaji wa deni la nje, ambalo linakadiriwa kufikia dola bilioni 1.3 kila mwaka ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, limesalia kuwa tatizo kubwa katika hifadhi ya kimataifa.

Waendesha bodaboda wakiwa kando ya Barabara ya Jinja mjini Kampala, Uganda. Picha ya Abubaker Lubowa.

Jumla ya deni la nchi hiyo linafikia takriban kiasi cha dola bilioni 21, na inakadiriwa litakuwa kwa zaidi ya asilimia 53 ya pato la taifa kabla ya kupunguzwa kwake katika mwaka wa fedha wa 2024/25, (Julai-Juni).

Katika miaka ya hivi karibuni, Uganda imekuwa ikichukua kiasi kikubwa cha fedha ili kufadhili sekta ya nishati, usafirishaji na miundombinu mingine huku maafisa wakiongeza bei ya mafuta ili kupata fedha za kumaliza deni hilo.

Mtibwa Sugar: Tunaisubiri Young Africans
Abdi Banda: Wabongo wanathamini sana Maproo