Serikali ya Rwanda, imeionya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba uchokozi unaoendelea kufanywa na DRC kwa kutumia ndege za kivita kwenye anga na ardhi ya Kigali, ni lazima usitishwe.

Ofisi ya Msemaji wa Serikali ya Rwanda, imesema inahakikisha kwamba ndege ya kivita aina ya Sukhoi-25 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ilikiuka taratibu za anga ya Rwanda, kando ya Ziwa Kivu lililopo magharibi mwa Rwanda.

Paul Kagame (Julia), akiteta jambo na Felix Tshidekedi.

Ofisi hiyo, imesema vitendo hivyo vya uchokozi ni kinyume na mikataba ya amani iliyoafikiwa na kusainiwa jijini Luanda nchini Angola na Nairobi nchini Kenya ambayo kwa pamoja inanuia kuleta suluhu la mzozo wa mashariki mwa DRC.

DRC katika miezi ya hivi karibuni ilikabiliwa na mashambulizi ya waasi wa M23 (“March 23 Movement”), mashariki mwa DRC yaliyoleta mvutano na Rwanda inayotuhumiwa kuunga mkono kundi hilo la waasi, madai ambayo yanakanushwa vikali na Serikali ya Kagame.

Kocha JKU afunguka ishu ya Feisal Salum
Agizo la Waziri Mkuu: Mkurugenzi kizimbani matumizi Mabaya ya madaraka