Mawaziri watatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, ambao ni wanachama wa chama cha mgombea wa urais, Moise Katumbi wamejiuzulu baada ya rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi kutaka kufahamu watakao muunga mkono katika uchaguzi ujao. 

Tshisekedi aliwaita, mawaziri watano ambao ni wanachama wa chama cha Katumbi cha Ensemble pour la Republique ili kujua msimamo wao na ndipo Mawaziri hao wa mipango, uchukuzi na Naibu Waziri wa Afya walipowasilisha ombi lao la kujiuzulu. 

Mfanyabiashara maarufu na aliyewahi kuwa Gavana jimbo la Katanga, Moise Katumbi Chapwe. Picha ya Al-jazeera.

Aidha, Rais Tshisekedi, ambaye aliingia madarakani Januari mwaka 2019, tayari ametangaza kuwa ana nia pia ya kugombea muhula wa pili mwaka ujao na tayari ameanza kusema mipango sawa kwa ajili ya uchaguzi huo.

Kwa upande wake Mfanyabiashara tajiri, Moise Katumbi (57) ambaye aliwahi kuwa Gavana wa eneo lenye utajiri wa madini la Katanga, mapema mwezi huu (Desemba 2022), alitangaza kugombea nafasi ya rais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023.

Uhuru wa Habari ulindwe kisheria: Balile

 

Azam FC yamkana Fei Toto, yashangazwa kutajwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 29, 2022