Waziri wa Afya wa Malawi, Khumbize Chiponda amesema nchi hiyo itachelewea kufungua shule za umma katika miji miwili mikuu ya nchi hiyo ya Blantyre na Lilongwe, ili kujaribu kupunguza kasi ya ongezeko la vifo vya kipindupindu.

Chiponda, ameyasema hayo na kudai kuwa jumla ya idadi ya kesi na vifo imeongezeka hadi 17,824 na 595 tangu kesi ziliripotiwa mara ya kwanza Machi, 2022 na kiwango cha vifo kikiongezeka hadi asilimia 3.34.

Amesema, “Kutokana na kuendelea kuongezeka kwa visa vya kipindupindu na vifo katika miji ya Blantyre na Lilongwe, shule za msingi na sekondari katika miji hiyo miwili hazitaanza Januari 3 kama ilivyoshauriwa.”

Hata hivyo, Waziri Chiponda amefafanua kuwa Kipindupindu ni tatizo la kila mwaka wakati wa miezi ya mvua nchini Malawi amefafanua kuwa  Novemba hadi Machi, ambapo idadi ya vifo ni karibu watu 100 kwa mwaka ingawa mlipuko wa sasa unatarajiwa kuwa mbaya zaidi.

Idadi ya vifo ajali Lori la mafuta yafikia 34
Shule kutofunguliwa kutokana na kipindupindu