Upande wa mashtaka umedai kukamilisha upelelezi wa Kesi inayomkabili mmiliki wa Kituo cha michezo cha Cambiasso, Kambi Zuber na wenzake watano kwa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine kilo 34.89 ambapo washitakiwa hao wataendelea kubaki rumande hadi Januari 16, 2023.

Hayo yamesemwa na Wakili wa serikali Caroline Matemu leo Januari 2, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio, anayeisikiliza kesi hiyo.

Matemu amesema mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa idadi ya mashaidi na vielelezo.

Washitakiwa wengine ni aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba Muharami Sultan, Maulid Zungu, Said Mwantiko, John Andrew na Sarah Joseph wote wakazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Katika shitaka la kwanza inadaiwa kuwa Oktoba 27, mwaka 2022 maeneo ya Kivule wilayani Ilala, Dar es Salaam walikutwa na dawa za kulevya aona ya heroin zenu uzito wa kilogramu 27.10.

Katika shitaka la pili, washitakiwa hao wanadaiwa Novemba 4, mwaka 2022 maeneo ya Kamegele Mkuranga mkoani Pwani, walikutwa na dawa hizo zenye uzito wa Kilogramu 7.79.

AU yaitaka Rwanda kutowaunga mkono M23
Hii ndio sababu ya Bushoke kupotelea kusikojulikana