Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania Mwinyi Zahera ameonesha kuwa tayari kwa mapambano baada ya kukamilisha usajili wa baadhi ya Wachezaji wenye uzoefu na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Zahera alitangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania Mwezi Novemba mwaka 2022, na alitarajiwa kufanya maboresho wa kusajili wachezaji kupitia Dirisha Dogo, ambalo rasmi litafungwa Januari 16.

Hadi sasa chini ya Kocha huyo kutoka DR Congo, Klabu ya Polisi imekamilisha usajili wa wachezaji sita, ambapo miongoni mwa hao yupo mmoja kutoka DR Congo.

Wachezaji hao ni Mohamed Banka (Ruvu Shooting), Kelvin Sabato (Singida Big Stars), Daud Mbweni (Singida Big Stars), Ibrahim Hamad Hilika (Mafunzo), Ramadhan Chombo ‘Redondo’ (Geita Gold) na Mayala Henock (SM Sanga Balende).

Polisi Tanzania itarejea tena Dimbani Jumamosi (Januari 14) kwa mchezo wa Mzunguuko wa 20 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC itakayokuwa nyumbani Uwanja wa Majaliwa.

Adam Adam aibukia Ihefu FC
Kesi ya Mkurugenzi wa Jatu bado mbichi