Katika kesi inayomkabili Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Jatu Public Limited, Peter Gasaya (32), anayekabiliwa na shitaka la  kujipatia fedha tasilimu Sh bilioni 5 kwa njia ya udanganyifu, umedai upelelezi haujakamilika.

Kwa mujibu wa Habari leo Gazeti mtandao Wakili wa serikali Tumaini Maingu, ameeleza hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Francis Mhina.

Maingu amesema kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya

Wakili wa utetezi Kung’he Wabeya, aliiomba mahakama ahirisho fupi kwa sababu wanataka kuwasilisha hoja  kuhusu dhamana ya mteja wao.

Baada ya kusikiliza maombi hayo Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo na mshitakiwa ataendelea kubaki rumande hadi Januari 13, mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka inadaiwa kuwa katika terehe isiyofahamika kati ya Januari Mosi na  Desemba 31, mwaka 2021 ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, mshitakiwa akiwa  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jatu Public Limited, alijipatia Sh 5,139,865,733.00 kutoka  Saccos ya Jatu, akijinasibu kukizalisha  kiasi hicho cha fedha kwa kuwekeza fedha katika kilimo cha faida, wakati akijua  si kweli.

Sita waongeza nguvu Polisi Tanzania
Atuhumiwa kumuua binti yake kisa Sh 56,000Â