Saa chache baada ya Klabu ya Mtibwa Sugar kutangaza kuachana na Mshambuliaji wa Tanzania Adam Adam, Klabu ya Ihefu FC imefikia makubalino ya kumsajili mchezaji huyo.

Adam Adam, ambaye aliwahi kucheza soka nchini Libya katika Klabu ya Al Wahda, alikuwa na wakati mgumu wa kuonesha uwezo wake tangu aliposajiliwa Mtibwa Sugar mwanzoni mwa msimu huu, na hivyo kusababishwa kuachwa katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo.

Kwa mantiki hiyo Adam Adam anajiunga na Ihefu FC kama mchezaji huru, na huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Young Africans Jumatatu (Januari 16).

Ihefu FC imeweka kambi Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, kujiandaa na mchezo huo, ambao utatumiwa kama kisasi kwa upande wa Young Africans, ambayo ilipoteza kwa mara ya kwanza dhidi ya Mbogo Maji, baada ya kucheza michezo 49 bila kufungwa.

Jean Baleke: Ninasubiri ruhusa TP Mazembe
Sita waongeza nguvu Polisi Tanzania