Kikosi cha Simba SC kimeanza safari ya kurejea nchini Tanzania kikitokea Dubai-Falme za Kirabu, kilipokuwa kimeweka kambi ya majuma mawili.

Simba SC imethibitisha kuondoka kwa kikosi chake huko Dubai kwa kuweka picha za video katika Kurasa zake za Mitandao ya kijamii mapema leo Jumanne (Januari 17) majira ya asubuhi.

Taarifa iliyoambatana na picha hiyo imeandikwa: “Muda wa kurudi nyumbani Tanzania.

Kesho Jumatano tutakuwa Uwanja wa Mkapa kuwapa burudani Wanasimba kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City.”

Ikiwa Kambini Dubai-Falme za Kiarabu, Simba SC chini ya Kocha Mkuu Roberto Olivieira, ilicheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Dhafra FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kirabu, pamoja na Mabingwa wa Zamani wa EUROPA League CSKA Moscow kutoka Urusi.

Simba SC ilipoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Dhafra FC, kisha ikaambulia matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya CSKA Moscow.

Dhumuni la kuweka kambi nje ya nchi ilikua ni kukiandaa kikosi cha Simba SC kwa ajili ya Michezo ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi.

Simba SC itaanza harakati za kucheza Hatau ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mwezi Februari 2023, ikipangwa kundi moja na Raja Casablanca ya Morocco, AC Horoya ya Guinea na Vipers SC ya Uganda.

Afisa wa Polisi akiri kuwabaka wanawake 12
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 17, 2023