Baada ya kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ugenini, Kikosi cha KMC FC kirejea jijini Dar es salaam na kuanza maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wa 21 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC.

KMC FC Ijumaa (Januari 13) ilicheza katika Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, Januari 24 itakua mwenyeji wa Namungo FC katika uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es salaam.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Klabu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni Christina Mwagala zinaeleza kuwa, kikosi chao kimeanza maandalizi hayo leo Jumatatu (Januari 16).

“Tumeanza leo maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya Namungo, utakuwa mchezo mgumu kutokana na kwamba kila mmoja anataka kufanya vizuri kwenye michezo hii iliyobakia kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2022/2023 hivyo kama Timu tuna muda wa kujiandaa vizuri.”

Katika maandalizi hayo KMC FC inawakosa wachezaji watatu kutokana na sababu ya majeraha ambo ni Ibrahimu Ame, Awesu Ally Awesu pamoja na Hance Masoud Msonga huku Emmanuel Mvuyekure akiendelea vizuri na hivyo muda wowote atajiunga na wenzake ili kuongeza nguvu kwenye michezo iliyobakia.

Aidha mbali na wachezaji hao wengine waliobakia wamerejea wakiwa na hali na morali ya kujiandaa vema dhidi ya Namungo na hivyo kuhakikisha kwamba Timu ya Manispaa ya Kinondoni inafanya vizuri kwenye michezo iliyobakia.

“Ukiangalia kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) tutakuwa na muda mrefu wakufanya maandalizi kabla ya mchezo wetu dhidi ya Namungo kutoka leo Januari 16 hadi 24 na kwamba program ya kocha Mkuu Hitimana itakuwa ni kufanya mazoezi ya uwanjani, Bichi pamoja na kucheza mechi za kirafiki ambazo zitasaidia kuwaweka sawa wachezaji kwa kipindi hiki tukiwasubiria wapinzani wetu.” amesema Christina Mwagala

Hadi sasa KMC FC imeshacheza jumla ya mechi 20 ikiwa imebakiza michezo 10 na hivyo kukusanya jumla ya alama 23 huku ikiwa kwenye nafasi ya tisa mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara na kwamba malengo ni kuhakikisha kwamba Timu inafanya vizuri kwenye michezo iliyobakia na hivyo kumaliza msimu kwenye nafasi nzuri.

RC Babu atoa maagaizo kwa wataalamu wa afya
Waziri Bashe amtimua mkandarasi