Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameanza Ziara mkoani Ruvuma na ametembelea mradi wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji unaojengwa katika kata ya Muhukuru Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Waziri Bashe hajaridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa skimu hiyo na amemuagiza Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa kumsimamisha na kuvunja mkataba na Mkandarasi huyo kwa utaratibu za kimkataba na kumpata mkandarasi mwingine ndani ya siku 30.

“Tafuteni mkandarasi mwingine ndani ya siku 30 awe site nataka mkandarasi atakayefanya kazi kiangazi na masika huyu hawezi hii kazi” amesema Bashe.

“Mimi sitaki hizi stori tunazoambiana kwamba tunabebana kwasababu sisi ni watanzania mpe kazi mtanzania kama anauwezo hana uwezo usimpe kazi kwa hoja ya utanzania irigation imekuwa chaka la watu kwa muda mrefu sana”.

“Enginia wa mkoa angalia uwezo unaopatikana hapa kwamba tunaweza kupata jumla ya hekta ngapi za watu kufanya shughuli za kilimo uhakiki ufanyike wa mradi huu badala ya kutegemea tuu mto muangalie muanze kubuni hata kama hatutajenga mwaka huu lakini kubuni ni wapi inaweza kujengwa”.amesema.

“Huyu bwana vunjeni mkataba ndani ya siku 30 tafuteni mkandarasi mwingine aje afanye hii kazi tusipotezeane muda fanyeni tathimini ya kazi aliyoifanya ya milioni 137 iko wapi?. na huu mradi ukamilike kama bajeti ilivyotaka kwahiyo watafutwe watu wa kuufanya huu mradi” amesema.

KMC FC yaitafutia dawa Namungo FC
Mwingine atambulisha Simba SC