Mamlaka ya Makumbusho jijini Berlin, imesema iko tayari kurudisha mamia ya mafuvu ya vichwa kutoka nchi za Afrika Mashariki, ambazo zilikuwa chini ya ukoloni wa Ujerumani.

Hatua hiyo, inakuja baada ya kuyafanyia utafiti mafuvu zaidi ya 1,000 kwa miaka kadhaa na kutambua asili yake ambapo mafuvu 904 kati ya hayo huenda yakapelekwa Rwanda, 202 Tanzania na 22 nchini Kenya.

Hata hivyo, watafiti hao hawakuweza kutambua asili ya mafuvu mengine saba na kulingana na wakfu wa urithi wa Kitamaduni wa Prussia, idadi kubwa ya mafuvu hayo yalitolewa makaburini.

Aidha, inaarifiwa kuwa pia baadhi ya mafuvu hayo yalitoka sehemu zilizokuwa zikitumiwa kufanya mauaji na mengine yalitokana na mauaji yaliyofanywa na Wajerumani kipindi cha ukoloni.

Arsenal yajitosa kwa Leandro Trossard
Wauawa kwa kukatwa mapanga, mmoja aondolewa sehemu za siri