Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Wanawake wawili kwa kutumia mapanga, akiwemo Bigile Mweshemi (53), ambaye aliondolewa sehemu za siri na wauaji hao.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Jamhuri Wiliam amesema tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Nyabulanda alfajiri ya Januari 16, 2023 wakati mama huyo akiwa shambani kwake naku kudai kuwa chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na imani za kishirikina.

Amesema, “aliondoka na kwenda shambani alfajiri kwa hiyo hao wakata mapanga walimvamia na kumkata na mbaya zaidi wakaondoka na sehemu za siri mambo mengine yanatisha ndugu zetu hawa wana mambo magumu sana.”

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi na kuongeza kuwa, “mmoja anayeshukiwa ambaye ni ndugu wa karibu waliyekuwa na mgogoro wa shamba kwa sasa ametoweka na wanaendelea kumsaka huyu ndiye anaedaiwa kuwatuma wakata mapanga.”

Katika tukio la pili, mkazi wa Kijiji cha Nyugwa, Melesiana Shija (70), aliuawa kwa kukatwa mapanga na mtu ambaye anahisiwa kwenda kwa mganga kabla ya baadaye kutekeleza mauaji hayo kisha kutoroka kusikojulikana.

Ujerumani yapanga kurejesha mafuvu ya vichwa Afrika Mashariki
Mamlaka za maji zatakiwa kujenga, kusimamia miundombinu