Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango amezitaka Mamlaka za Maji pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo kuongeza weledi katika usimamizi wa rasilimali za maji kwa kujenga miundombinu mingi zaidi ya kutunza na kuvuna maji ya mvua, ili kukabiliana na changamoto za maji.

Dkt. Mpango ameyasema hayo hii leo Januari 19, 2023 mjini Shinyanga wakati akiweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria utakaohudumia Tinde na Shelui na unaotarajia kugharimu shilingi bilioni 24.4.

Amesema, watendaji hao wanatakiwa kuongeza ufanisi wa matumizi ya maji hasa kwenye kilimo na kutunza vyanzo vya maji ikiwemo cha Ziwa Victoria kilichopo Ihelele Wilayani Misungwi, ambacho ni tegemeo kwa huduma za maji katika Miji ya Wilaya za Misungwi, Kahama, Shinyanga, Tabora, Kahama, Nzega, Igunga, Shelui na Tinde.

Aidha Dkt. Mpango amesema dhamira ya Serikali ni kuona mradi huo unatoa maji na kuwa endelevu kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na pia juhudi za kupeleka maji katika maeneo yaliyopo karibu na mradi huo zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maeneo yote yanapata majisafi na salama na yanatosheleza mahitaji.

Wauawa kwa kukatwa mapanga, mmoja aondolewa sehemu za siri
Msako wa wezi vifaa vya SGR waanza