Takriban Watu 18 wamefariki baada ya Helikopta ya Polisi kuanguka kwenye jengo la chekechea lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Ukraine Kiev, ambapo Rais wa nchi hiyo, Volodymyr Zelensky amesema ajali hiyo ni msiba mkubwa.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Denys Monastyrsky, Naibu wake na Waziri wa nchi ni miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo na tayari uchunguzi juu ya tukio hilo ili kubaini chanzo chake unaendelea.

Mabaki ya Helikopta iliyopata ajali nchini Ukraine. Picha ya POLITICO.

Naibu Mkuu wa ofisi ya rais mjini Kiev, Kyryolo Tymoshenko amesema katika ajali hiyo watoto watatu pia walifariki na wengine 15 wamejeruhiwa na kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikisafiri kuelekea mstari wa mbele wa vita.

Viongozi mbali mbali wa Ulaya, wametuma salamu zao za rambirambi, huku Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akisema mkasa huo unadhihirisha gharama kubwa inayolipwa na Ukraine, katika vita vya uvamizi wa Urusi.

Singida Big Stars yawashangaa mashabiki
Mbeya City wapinga kadi nyekundu, penati