Baada ya kushinda kesi dhidi ya Shirikisho la Soka Barani Ulaya ‘UEFA’, viongozi wanaounda Michuano mipya ya ‘European Super League’ wamesema wapo katika hali nzuri.
Viongozi hao wamesema mpaka sasa timu 50 zimethibitisha kushiriki michuano ikiwemo Real Madrid, FC Barcelona na Juventus ambao ni waasisi wa michuano hiyo.
Hata hivyo Rais wa Klabu ya Real Madrid Frontino Perez ambaye ni sehemu ya viongozi wa ‘European Super League’ amesema wanatazamia michuano hiyo itashirikisha klabu zaidi ya 60-80.
Mfumo wa michuano itakuwa katika hatua 4 na hakuna timu itayokuwa maalumu na kila timu itacheza michezo 14 kila msimu.
Wazo wa Michuano ya European Super League lilianikwa hadharani Aprili 2021 ikiwa na waasisi kuni na mbili ambao ni Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Tottenham, AC Milan, Inter Milan, Juventus, Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid.