Mwamuzi kutoka Algeria Mustapha Ghorbal ameteuliwa kusimamia mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia la FIFA ngazi ya Vilabu, kati ya Mabingwa wa Ulaya Real Madrid dhidi ya mabingwa wa Asia Al Hilal (Saudi Arabia).

Mchezo huo utachezwa Februari 11, 2023 katika dimba la Prince Moulay Abdellah Mjini Rabat Moroco majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mwamuzi Mustapha Ghorbal

Real Madrid ilitinga fainali baada ya kuwalaza miamba ya Misri Al Ahly bao 4-1 huku Al Hilal ikifikia hatua hiyo kufuatia ushindi wa 3-2 dhidi ya miamba ya Brazil, Flamengo.

Al Ahly na Flamengo zitachuana kutafuta mshindi wa tatu Februari 11 katika dimba hilo majira ya saa 12:30 jioni.

Spika Tulia afafanua na kuifuta kauli ya Mwigulu
Msamaha wa ruzuku hutolewa kwa umuhimu: Majaliwa