Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema lengo la Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kuhusu wabunge kumuacha ajadili masuala ya uchumi na wao wajadili uganga wa kienyeji lilikuwa ni kumjibu Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina.

Dkt. Tulia ameyasema hayo hii leo Februari 9, 2023 wakati akijibu utaratibu uliombwa na Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba baada ya Mbunge wa Tandahimba (CCM), Katani Katani akichangia taarifa za kamati Bungeni, huku akitangaza kufutwa kwa kauli hiyo katika kumbukumbu rasmi za Bunge.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

Katika matamshi yake Bungeni, Mwigulu, alisema “Embu tujadili mambo mengine yanayohusu uganga wa kienyeji kwenye uchumi hii ni taaluma yangu, mnajadilije vitu ambavyo viko wazi,” na kauli hiyo kujibiwa na Katani kuwa waziri huyo amewatukana wabunge.

Dkt. Tulia amesema, ni kweli Waziri Mwigulu alitamka kauli hiyo bungeni, iliyowafanya baadhi ya wabunge kuirejea kwa mtazamo hasi na kudai kanuni ya Bunge ya 71 inataka wabunge kutumia lugha ya staha wakati wakiwa bungeni.

European Super League yajimwambafai
Pilato wa Algeria kuamua Fainali Kombe la Dunia