Rais William Ruto  amemuhamisha Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof. Kithure Kindiki kutoka katika ofisi yake Nairobi na kumpeleka eneo la North Rift ili kupambana na matukio ya ujambazi.

Ruto aliyasema hayo Februari 12 2023, wakati akieleza jinsi alivyo muamuru Prof. Kindiki kutoka katika afisi ya Harambee Avenue, hadi eneo lililokumbwa na ukosefu wa usalama ambapo anatarajiwa kurejesha usalama.

“CS Kindiki hayupo hapa leo kwa sababu alikuwa Baringo, na akaelekea Turkana Nimemwambia aondoke ofisini kwakwe Nairobi aende akaishi North Rift hadi ujambazi utakapokamilika,” alisema Ruto.

Rais wa Kenya, William Ruto. Picha ya NMG.

Alisema,”tuweka mikakati mingi ya kupambana na ujambazi katika siku zijazo, na kwamba atahakikisha hakuna maisha ya raia wake yanayopotea, kupitia mashambulizi ya majambazi tutashughulika na watu hao wachache wenye kiburi na kuhakikisha hakuna Mkenya anayepoteza maisha kwao,” alisema Ruto.

Wezi wa ng’ombe na majambazi, wamesababisha uharibifu katika eneo la North Rift nchini, na kusababisha hasara ya mamia ya maisha, kuhama kwa wakaazi, na kupoteza maelfu ya mifugo.

Kaunti zilizoathiriwa zaidi ni Baringo, Turkana na Elgeyo Marakwet. Siku mbili tu zilizopita, mnamo Ijumaa, watu sita, miongoni mwao maafisa wanne wa polisi, walipoteza maisha katika shambulio la majambazi kwenye barabara kuu ya Kitale – Lodwar eneo la Kaakong Kaunti ya Turkana.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki.

Wakati huo huo, maafisa saba, akiwemo Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo, walilazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi katika ufyatulianaji risasi uliodumu saa moja usiku na mapigano hayo ya risasi yalirekodiwa na abiria wakati magari yaliyokuwa yakisindikizwa na polisi, na kuwaonyesha majambazi wapatao 300 msituni.

Hata hivyo, matamshi ya Rais Ruto yanafuatia hisia za gavana wa Trans Nzoia George Natembeya kwamba ustawi wa maafisa wa polisi waliotumwa katika eneo hilo lenye matatizo ni mbaya ambaye pia alisema mengi yanafichwa kuhusiana na masharti wanayowekewa maafisa na jambo hilo limepuuzwa kabisa.

“Nilikuwa Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa na nilipigana bila usalama kuna mambo hutaambiwa kamwe Rais . Katika kipindi cha miaka mitatu kama RC sikupokea hata senti moja ya kupambana na ukosefu wa usalama, hawa maafisa tunaowaona wanauawa kwa kupigwa risasi, na hakuna hata mmoja wao anayepewa posho, mshahara anaopata ni sawa na afisa wa trafiki, hakuna motisha yoyote,” aliongeza.

TCRA kuzima laini za simu zisizo hakikiwa
Muumini adai zaka Kanisani, asema ameghairi kwenda Mbinguni