Vitabu 16 vilivyobainiwa kukiuka mila na desturi za kitanzania vimepigwa maruku kutumika au kuonekana ndani ya shule yeyote nchini na Taasisi za Elimu nchini.

Waziri wa elimu Sayansi na Teknojia Prof. Adolf Mkenda, amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalam wa Wizara hiyo, imezibaini shule kadhaa kutumia vitabu vinavyo kinzana na utamaduni wa kitanzania.

Waziri wa elimu Sayansi na Teknojia Prof. Adolf Mkenda.

Amesema, anasitisha matumizi ya vitabu hivyo chini ya kifungu cha 59 cha sheria ya elimu sura ya 353, iliyompa jukumu hilo.

Wizara hiyo, pia imezitaka shule zote za Awali, Msingi na Sekondari ziwe zinazotumia mitaala ya ndani au ya nje ya nchi, zitekeleze masharti yaliyoainishwa kupitia waraka wa elimu namba 4 wa mwaka 2014.

Serikali kuweka mazingira wezeshi sekta ya utalii
Tanzania kunufaika na Bil 120 miradi uhifadhi wa Mazingira