Taarifa za ajali ya ndege iliyoripotiwa kutokea hii leo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, si za kweli bali ni ilikuwa ni jaribio la kupima utayari wa kuokoa pindi ajali za ndege zinapotokea na hakuna tukio la vifo wala majeruhi.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amesema zoezi hilo liliratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili ambazo kwa awamu hi ilikuwa ni Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.

Amesema, “Tulipokea taarifa ya ajali ya ndege tukafika eneo la tukio tukaja kutambua ni zoezi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kujipima utayari wa kuokoa, walifanya hilo zoezi kwa usiri mkubwa sana kwasababu wote tulifika hapa.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amevishukuru vyombo vyote vya ulinzi na usalama vya Kahama kwa utayari na kujitoa kufika kwa wakati eneo la tukio kitu ambacho kimeonesha kuwa wapo makini katika kutekeleza majukumu ya kikazi.

Majeruhi wa kuigiza wakati wa ajali hiyo.

Awali akizungumzia tukio hilo, Meneja wa uwanja wa ndege Wilaya ya Kahama, Hamza Kiyemo amesema wamefanya tukio hilo la utayari wa jaribio la ndege kuwaka moto, ili kujiweka sawa endapo ajali ikitokea kweli, wawe na utayari wa kufanya uokoaji wa maisha ya abiria na vitu.

Tukio hilo, lilifanyika hii leo Februari 13, 2023 jirani na uwanja wa ndege wa Kahama kwa kuwashwa moto mfano wa ndege iliyoungua, pamoja na baadhi ya watu kuigiza kuwa wamepata ajali huku magari ya Zimamoto na ya wagonjwa wakipishana hali iliyoleta taharuki.

USCAF yawamulika wanafunzi mahitaji maalum
Tanzania, Indonesia kushirikiana sekta ya Umeme Mafuta na Gesi