Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka amekemea baadhi ya watumishi ambao wamekua sio waadilifu kwa kuendekeza rushwa jambo linalochangia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi Wilayani humo.

Shaka, ameyasema hayo katika Baraza la Madiwani Wilayani humo na kuongeza kuwa baadhi ya watendaji wa Vijiji, Kata, Madiwani na Watumishi wamekua kikwanzo cha Serikali kukomesha changamoto hiyo kwa kuchukua rushwa kwa wafugaji na wakulima wahalifu.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka.

Amesema, katika uongozi wake hatakubali kumvumilia kiongozi ambaye atakua chanzo cha migogoro kwa kuendekeza rushwa, na kudai malalamiko mengi yanayoletwa na wananchi yanababishwa na kukosekana Kwa uadilifu Kwa viongozi Jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kimaadili.

“nimekaa muda mfupi wa wiki MBili hapa Kilosa nimegundua migogoro ya ardhi inasababishwa na viongozi kukosa uadilifu na uzalendo Kwa kuendekeza vitendo vya rushwa Hivyo sitamvumilia Mtendaji atakayekua kikwanzo,” amesema Shaka.

Mbeya waja na mkakati ajira kwa Vijana sekta ya Madini
Ramaphosa agoma AKA kufanyiwa mazishi ya kitaifa