Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2022/23 ameridhia kuipatia Wizara Shilingi Bilioni 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa.
Waziri Ulega ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la maji la Kwekinkwembe Wilayani Kilindi Mkoani Tanga na kumtaka Mkandarasi kuhakikisha anatoa taarifa ya kila hatua ya ujenzi na kuacha nakala Wilayani hadi ngazi ya kijiji na kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Busalama amewataka wananchi wa Kijiji cha Kwekinkwembe kuhakikisha wanalisimamia vyema bwawa hilo, linalojengwa kwa thamani ya Shilingi Bilioni 504, ili liwe na tija kwao.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini – CCWT (W) Kilindi Mkoani Tanga, Merieki Long’oni amesema ni faraja kwao kuona Serikali inawasogezea huduma ya maji karibu kwa ajili ya mifugo yao kutokana na uhaba wa hitaji hilo katika baadhi ya maeneo ya Wilaya hiyo.